John 17:1-5

Yesu Ajiombea Mwenyewe

1 aBaada ya Yesu kusema haya, alitazama kuelekea mbinguni akawaombea na kusema:

“Baba, saa imewadia. Umtukuze Mwanao, ili Mwanao apate kukutukuza wewe.
2 bKwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa. 3 cNao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. 4 dNimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye. 5 eHivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujakuwepo.

Copyright information for SwhNEN